
Elimu kambini Gasorwe
Katika Kambi ya Gasorwe tuna shule za watoto wachanga (Maternelle), za watoto wakuinukia (Primaire) na hata shule ya Sekondari. Kuongeleya elimu katika kambi ya Gasorwe ni muhimu sana kwa sisi wote tunaoishi humu na wote waliopitiya humu. Elimu tuliopata tangu mwanzoni hadi sasa imekuwa ni chanzo cha maendeleyo makubwa sana na mafanikio wa wengine.
Baada ya watu tuliokuwa tukihamishwa toka kambi za muda(Camps de transit) kuonekana kuwa idadi ilikuwa inazidi kuongezeka, hitaji ya kupata elimu ikawapo ndipo UNHCR na wadau wengine walipoanzisha shule na kwa hiyo watoto wakaanza kusoma. Mwanzoni kuna madarasa ambayo hayakuwepo, bali yalikuja kuongezewa kadiri ya vile tulivyosonga mbele katika myaka ya shule. Kwa mfano darasa la mwaka wa mwisho wa sekondari lilikuja kuongezewa nyuma.
Kutokana na uhaba wa vipengle vya kusoma, ilibidi kwa wale watoto waliokuwa wakionekana kuwa wazoefu zaidi kwenda kusomeya Jijini Bujumbura kwenye shule ya Ubalozi wa Congo. Na mchakato huo uliendelya hadi myaka ya hivi nyuma wakati hayo yalipofikia mwisho na hata kusimamishwa.