Mwanzo wa Kambi ya Gasorwe
Kambi ya Gasorwe au Kambi ya Wakimbizi ya Gasorwe, ni Kambi ambayo inawahifadhi Wakimbizi wa asili ya Kikongomani ikiwa inapatikana katika Mkoa wa Muyinga tarafani Gasorwe kwenye milima ya Kinama na Bihogo.
Kambi hii imeanzishwa kwa ajili ya kuwahifadhi wa kumbizi waliokuwa wakitoroka vita nchini Congo ya Kidemokratia. Ilianzishwa mwaka wa 2002. Mwanzoni ilikuwa na uwezo wa kuwapokea watu wasiyo wa idadi ya juu zaidi, bali kutokana na hali ilivyokuwa ikiwapelekea watu kuyahama makazi yao na hivyo kupata mahali pa usalama Nchini Burundi, ilizidi kungezewa uwezo. Kwa hesabu kamili ya watu ambao walianza hatuna uhakika. Bali tujuavyo ni kwamba tangu mwaka wa 2002 kambi hii ilikwa na qurtiers 13 tu.
Kwa sasa kambi ya Gasorwe imefikia idadi ya quartiers ni 40. Na hata watu wenyewe kugawa majina kutokana na sehemu ambazo wanaziishi. Na tukilinganisha na ukubwa wa idadi iliyoanza na iliyopo kwa sasa ya quartiers, tunaona kwamba kambi hii imepata muongezeko mkubwa zaidi.
Kueleza yote yanayohusu kambi ya Gasorwe ni mhimu sana katika maisha yetu na zaidi kwa wale wote waliofika nyuma ao watoto ambao wanazaliwa kwa sasa.
Mwanzoni, kambi ya Gasorwe, kwa kuwa ilikuwa na idadi ndogo sana ya watu, tulikuwa na usalama zaidi wa chakula. Wakati huo tulikuwa na aina mbali mbali za chakula : Samaki, Nyama, Sombe kwa wingi, viyazi, ...
Watu wengi walioishi kipindi hicho, kumbukumbu bado ni nyingi na hata kupelekeya wengi pia kuelewa kwmba manadiliko ya hali ya hewa yameleta madiliko makubwa.
Huduma za wadau zilikuwa za kutosha zaidi, na hiyo inaeleweka kwa sababu kambi hii ilikuwa bado mpya na idadi ya wakimbizi Ulimwenguni kwote haikuwa kama siku hizi za nyuma.
Kambi Gasorwe, tuliwapata wadau ambao hata sasa tulibaki na kumbukumbu zao kwa kuwapa watoto wetu majina yao.
Vipindi hivyo vya mwanzoni vilikuwa na vya raha kubwa zaidi na maisha yalikua yakuburudisha. Tulikuwa tukilietewa viatu, mavazi, ...
Pia, nyakati za sherehe kubwa za mwisho wa mwaka au sikukuu za Wakimbizi Ulimwenguni, tulikuwa tukipata huduma zisizo za kawaida na watu walipata faraja zaidi nyakati hizo na hata ikawa ni mojawapo ya huduma zilizowapelekeya watu kupata upungufu magumu yaliyowapata nyakati za shida wakitoraka vita.
Kambini Gasorwe tumepitia nyakati ngumu pia; ilipofikia ambapo sisi wenyenwe hatukuwa na maelewano, ilikuwa vigumu kuelewa tena kile kilichokuwa kikiendelea kwa wakati huo. Shukrani kwa Mungu sababu baada ya hizo hali zote za kutokuelewana, hii leo hali ni ya usalama.
Maisha ya Kambini ni ya kambini, ila kwa yote tuliyoyapitia na kuyapata kabini Gasorwe, leo wengi wetu tumekuwa watu walioelimu na hata kupata uweza mbalimbali wa kazi. Tumewapata viongozi mbalimbali ambao kwa uweza wao kama binadamu waliwezesha pia maendeleo na kuzingatia kambi yetu. Waalimu mbalimbali wenye kiwango cha mafunzo kilicho cha juu wamewezesha elimukambini humu kuzidi kuwa bira zaid na hata kupata wanafunzi kutoka hapa kambini ambao wametenda vema sana hata walipoelekea kwenye shule la ubalozi wa Congo, mjini Bujumbura.
Uongozi
Kambi ya Gasorwe au Kambi ya Wakimbizi ya Gasorwe, inasimamiwa na shirika la serekali liitwalo ONPRA, kwa sasa ila hapo mbeleni halikuwepo. Tunahudumiwa na UNHCR, na wadau wengine mbali mbali.
Kambi hii inaongozwa na kamati ya wakimbizi ambayo inasimamiwa na Mkuu Wa Kambi.
Ukurasa wa viongozi wote ambao walitawala kambi yetu uko hapa
Elimu
Kambi ya Gasorwe au Kambi ya Wakimbizi ya Gasorwe, ina shule ya watot wadogo sana "Kipusa", na shule ya msingi na shule ya upili.
Katika historia ya shule hizo, tumepata waalimu wengi na wa ujuzi tofauti. Miongoni mwao tuna mwalimu mkongwe, Muhasha Bitingingwa, Mukome Kabemba Leonard ambao hadi sasa sifa na umaarufu wao waendeleya. Na zaidi ya wazee hao kuwa waalimu, waliaminika kuwa na wengi kuwa wazee wa busara na washauri wakubwa. Hadi sasa shuhuda zao zadumu.
Tumewapata viongozi mbalimbali wa shule hizi ambao tutaingilia kiundani zaidi.
Ukurasa wa waalimu wote upo hapa
Maendeleo
Ili kupata maendeleo zaidi temebeleya kipengele chetu cha vipaji. Fahamu mengi hapa
