


Vipaji
Vipaji Kambini Gasorwe
Fahamu wenye vipaji wa kambi ya Gasorwe pamoja na Weka Gasorwe. Kambini Gasorwe tuna wenye vipaji wengi na ni vipaji mbalimbali.
Kwenye Wikipedia Kipaji kinatafsiriwa hivi :
Kipaji (kutoka kitenzi "ku-pa"; kwa kuwa watu wa dini huamini kipaji mtu hupewa na Mungu katika uumbaji) ni sehemu ya uwezo wa kufanya jambo fulani kwa ngazi ya juu. Kipaji kinaweza kuwa cha kimwili au cha kiakili.
Kipaji ni uwezo wa kuzaliwa nao wa kufanya kazi fulani lakini kinaweza kikandelezwa au kutoendelezwa. Kipaji hakirithishwi wala huwezi kujifunza sehemu yoyote. Ni uwezo, ujuzi ulioendelezwa, maarifa au uhodari na mtazamo alionao mtu.
Asili ya ndani ya kipaji ni kuonyesha ujuzi na mafanikio, ambayo huwakilisha maarifa au uwezo unaopatikana kupitia kujifunza.
Kipaji huweza kuishi ndani ya mtu bila kupotea. Kadiri kinavyozidi kutumiwa ndivyo huzidi kuimarika. Mfano wa vipaji ni: kuchora, kutambua na kuvumbua vitu kwa haraka.
Kwa hiyo tunaona kwamba unaweza ukawa na kipaji na hicho ni tangu kuzaliwa hadi mwisho wako utabaki nacho. Pia wataalamu wanatuambia ya kwamba kila mtu ana kipaji chako. Hapo tunaona pia kwamba kuna sehemu nyingine muhimu sana ya kutambua kipaji chako. Bali kama kama ukupata fursa ya kuendeleya kujifunza zaidi hiyo inasababisha kukifanya kipaji chako kiimarike zaidi. Na hilo ndilo lengo letu hapa kuvipandisha vipaji vya Kambini Gasorwe. Fwata video mbalimbali