Kambi zingine
Nchini Burundi na Ulimwenguni kote, Kambi yetu ya Gasorwe haiko peke yake. Kadiri tulivyokimbia vita nchini mwetu tukaja kambini Gasorwe, kuna wengine wengine ambao pia walivitoroka vita sehemeu mbalimbali Nchini kwetu na sehemu zingine duniani. Ni vema kupata ufahamu wa kambi zingine za hapa Burundi na kwengine kote ulimwenguni. Kwa sasa tutaongeleya kambi tu za hapa Nchini Burundi.
Miongoni mwa kambi za kudumu za wakimbizi Wakongomani hapa Nchini Burundi, Kambi ya Gasorwe ndiyo ilikuwa ya kwanza. Ilianza hapo mwaka wa 2002 na hadi sasa ina idadi kubwa ya watu. Iliyotwata ilikuwa ni Kambi ya Mwaro ambyo haipo tena kwa sasa ilia waliokuwa huko walihamishwa wakapelekwa Bwagiriza. Kambi iliyofwata ni kambi ya Musasa. Na zingine zikafwata baadaye na ya mwisho ni Kambi ya Nyankanda.