top of page
  • White Facebook Icon
  • White Twitter Icon
  • White YouTube Icon
  • White Instagram Icon

Mukome Kabemba


Mukome Kabemba na Maman Loyi
Mukome Kabemba na Maman Loyi

Mzee Mukome Kabemba Léonard ni mmoja wa wazee tuliowapata kambini ambao walikuwa msaada mkubwa sana kwa vijana na kwa watu wote kwa jumla. Alikuwa mtu aliyependa watu wote, alikuwa mshauri na zaidi alipendelea kuwahimiza vijana kupenda masomo na hivyo kunufaika na elimu.


Kambini Gasorwe, Mzee Kabemba alikuwa na kazi ambayo ilimpelekea kufahamika vizuri zaidi. Na hiyo kazi yeye alikuwa Mwalimu wa shule. Alipofika kambini Gasorwe, alianza akiwa mwalimu kusaidia shule yetu Sekondari. Moja ya kozi alizozifundisha na ambayo alionekana kuwa na ufasaha mzuri zaidi ilikuwa ni kozi ya Hesabu. Alifundisha Hesabu kwa kipindi cha miaka kadha na hivyo akawasaidia wengi kusonga mbele. Baada ya muda fulani, Mzee Kabemba akiwa na rafiki yake msiri na wa sana aliyeitwa Mzee Muhasha, walishushwa kwenye shule ya Msingi ya hapa Kambini Gasorwe, na wote wawili wakapewa darasa la sita kila mmoja na lake. Walisaidiya kwa mara nyingine tena kwa kuwezesha watoto wetu wa hapa kambini kuelimika zaidi na hivyo kufaidiak kwa ule ujuzi waliokuwa nao hawa wawili.

Walianzisha kitu ambacho hapo mwanzo kilikuwa bado kutendeka kwenye shule yetu ya msingi, kwa kuleta mfumo mpya kabisa wa kumupa kila mwalimu kufundisha kozi anayojisikia kuwa na kina zaidi na hivyo kuboresha zaidi usikivu na ufahamu wa watoto. Mzee Kabemba alifundisha Kozi ya Hesabu kama alivyofundisha pia kwenye sule ya Sekondari naye Mzee Muhasha ambaye alikuwa na uzoefu mkubwa sana wa Lugha ya Kifaransa akawa na Kozi hiyo ya Kifaransa. Na zile kozi ndogo ndogo walizigawana kati yao. Kwa kweli watoto waliosoma wakati huo walikuwa na elimu ya kiwango cha juu na hadi leo shuhuda ni nyingi sana. Kipindi walichokifanya kwenye shule ya Sekondari na kile walichokifanya kwenye shule ya Msingi, waliweza kuonesha uzoefu wa hali ya juu na kupelekea wamoja kuwaona kama watu ambao alileta mabadiliko makubwa sana katika elimu katika shule zetu ya Misnig na ile ya Sekondari.


Habari za Mzee Muhasha zitafuata katika sehemu yake binafsi.


Mzee Mukome Kabemba alikuja kambini Gasorwe tangu mwaka wa 2002, aliishi humo hadi mwaka wa 2018 alipofariki kutokana na magonjwa. Alipotoka kwenye shule ya Kambini Gasorwe, alipata kazi nyingine tena ya walimu pia na kuanza kundisha kwenye shule ya msingi Mjini Bujumbura, ambayo ni shule ya Ubalozi wa Congo hapa Nchini Burundi. Alianza kufundisha darasa la sita na halafu akawekwa baadaye katika darasa la nne. Na hadi wakati alipoiaga dunia.


Mukome Kabemba akiwa shuleni
Mukome Kabemba akiwa shuleni

 
 
 

Comments

Couldn’t Load Comments
It looks like there was a technical problem. Try reconnecting or refreshing the page.
bottom of page